WAZIRI MKUU: HAKUNA MAKINIKIA YANAYOUZWA BILA KULIPIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema makinikia yote yanayosafirishwa yamefuata taratibu na hakuna makinikia yanayouzwa bila kulipiwa kwanza. “Makontena yote yanayosafirishwa hivi sasa, tayari yameshauzwa na kulipiwa na fedha iko kwenye akaunti zetu. Hapo yako chini ya mnunuzi na yeye yuko huru kuyapeleka anakotaka. Kwa hiyo, Watanzania hatupati hasira. Nataka niwaondolee hofu ya awali… makontena hayo